Utalii wa Matibabu huko Bangalore India
Hospitali za Apollo, Bengaluru, wametunukiwa cheti cha JCI, wanatoa huduma ya afya ya kisasa zaidi kwa kutumia teknolojia za kisasa, na wakittoa huduma hizo kwa wagonjwa kutoka nchi mbalimbali. Hospitali imejidhatiti kuwekeza katika teknolojia za kisasa za afya sanjari na maendeleo ya kiteknolojia ya dunia, yote hiyo ni ili kuhakikisha kwamba wagonjwa wanafaidika na maendeleo hayo.
Ikiwa na ukubwa wa zaidi ya sqft 212,000 katika mazingira mazuri, hospitali yetu ina vitanda 250 kwa wagonjwa wanaolazwa. Katika utafiti uliofanywa wa Best Hospital Survey mwaka wa 2013na THE Week-A C Nielsen, Hospitali za Apollo zilishika nafasi ya 2 kwa kuwa hospitali bora zinazotoa huduma pekee Bangalore.
Mbali na kuwa Kituo cha Ubora kwa kuwa na Kituo cha Minimal Access Surgery (MASC) kwa ajili ya kufanya upasuaji wa kidogo aina ya invasive surgeries, hospitali imefanikiwa kuongoza kufanya upasuaji ngumu zaidi kama Spinal Angiolipoma Excision, Tibial Tuberosity Shift na MPSL reconstruction na kufanya implantation of four autologous chondrocyte.
Hospitali ina wataalamu bora wa afya pamoja na washirika wengine wanaotibu wagonjwa na pia ni hospitali ya kwanza kutumia kifaa chenye muundo wa Y shape stent kwa ajili ya tracheoesophageal fistula katika eneo hilo.. Baadhi ya teknolojia inayotumika katika Hospitali za Apollo, Bengaluru:
- Thallium Laser-Ya kwanza India
- Holmium Laser-Ya kwanza Kusini mwa India
- Digital X-Ray- Ya kwanza Karnataka
- 64 slice CT angiogram
- 1.5 Tesla MRI
- Low energy & High energy Linear Accelerators
- Navigation System kwa ajili ya usahihi wakati wa upasuaji
- 4-D Ultrasound kwa ajili ya 4 dimensional sonography
- Digital Fluoroscopy
- Gamma Camera
Katika Hospitali za Apollo tunaelewa kuwa kutafuta matibabu nje ya nchi yako ni jambo linaloweza kukuhangaisha sana na kukusumbua kimawazo lakini tutakusaidia kupunguza hali hiyo. Turuhusu tukusaidie kupanga pamoja nawe safari kwa kujaza fomu iliyo upande wa kulia ili Msaidizi wetu wa Kimataifa akusaidie.
APOLLO HOSPITALS
Address: Bangalore 154/11,
Opp IIM, Bannerghatta Road
Bangalore - 560076 (India)