Utalii wa Matibabu huko Kolkata Uhindi
Hospitali ya Apollo Gleneagles ni muunganiko wa Hospitali za Apollo Group, India na Parkway Health ya Singapore, ambayo inaongoza kwa kutoa huduma za afya katika bara la Asia. Ikiwa na vitanda 610, hospitali inatoa huduma ya matibabu mbalimbali kutia ndani yaliyo magumu kwa kutumia teknolojia ya kisasa na madaktari waliobobea.
Mbali na kuwa hospitali pekee Mashariki mwa India iliyotunukiwa cheti cha Joint Commission International (JCI) , ikiwa kitovu cha ubora, Hospitali ya Apollo Gleneagles inaendelea kupata NABL kwa: Clinical Biochemistry, Clinical Pathology, Haematology&Immunohaematology, Microbiology & Serology, Histopathology& Cytopathology.
Kwa kuongezea lengo lake la kufikia viwango vya kimataifa kwa faida ya wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali duniani, Apollo Gleneagles ilipokea ISO 22000:2005: HACCP Certification (mfano. Kupokea, kuweka akiba, kutayarisha na kupelkea chakula kilichopikwa na kisichopikwa kwa wagonjwa waliolazwa, wasiolaza na katika migaha ya chakula na vinywaji).
Apollo Gleneagles Cancer Hospital (AGCH), Kolkata, yenye vitanda 100 inatoa huduma bora kwa wagonjwa wa kansa. Ikiwa na vitanda 50 kwa ajili ya upasuaji wa wagonjwa wenye kansa, hospitali inajulikana kuwa hospitali bora ya Kansa Mashariki mwa India. Hospitali inatumia mbinu ya kuondoa kansa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya NovalisTx ya Brain LAB, teknolojia hiyo hupunguza uharibifu wowote unaoweza kutoka katika tishu ya mwili.
Katika Hospitali za Apollo tunaelewa kuwa kutafuta matibabu nje ya nchi yako ni jambo linaloweza kukuhangaisha sana na kukusumbua kimawazo lakini tutakusaidia kupunguza hali hiyo. Turuhusu tukusaidie kupanga pamoja nawe safari kwa kujaza fomu iliyo upande wa kulia ili Msaidizi wetu wa Kimataifa akusaidie..
Apollo Gleneagles Hospitals
Address: 58, Canal Circular Road,
Kadapara, Phool Bagan, ,
Kolkata, ,
West Bengal 700054, India.