International Patient Care

Search form

 

Utalii wa Matibabu huko Delhi India

Swahili
Pata Ushauri wa Daktari Mtandaoni

Hospitali ya Apollo Indraprastha, New Delhi ni kubwa ikiwa na vitanda 700 kwa ajili ya wagonjwa na ikiwa katika eneo lenye ukubwa wa sq ft 600,000 katika Mji Mkuu wa Nchi. Hospitali inajulikana kwa kuwa hospitali bora zaidi na ya kwanza nchini India kupokea cheti cha Joint Commission International (JCI)

Tangu ilipoanzishwa mwaka wa 1996, hospitali imeendelea kujali mahitaji ya wagonjwa na kuendelea kutoa huduma za afya za kiwango cha juu kwa kila mgonjwa.

Hospitali ya Apollo New Delhi inatumia kikamilifu uzoefu wake wa miaka 31 ambayo walitumia kutibu na kuaminia na wagonjwa zaidi ya milioni 41 duniani, kuwa na kiwango bora cha huduma kwa wagonjwa, kuboresha maisha ya wagonjwa na familia zao.

Kwa ufupi Hospitali ya Apollo, New Delhi imetimiza yafuatayo:

  • Inatoa matibabu ya kina katika aina 52 za pekee au Specialties
  • Hospitali ya kwanza nchini India kufanya upasuaji wa Paediatric Liver Transplant mwaka wa 1998 katika mojawapo ya programu yenye shughuli nyingi zaidi ya Upandikizi wa Ini na Figo nchini
  • Hospitali yenye Idadi kubwa ya vitanda kwa ajili ya hali ya dharura kati ya hospitali binafsi nchini India
  • Maabara zake zimetunukiwa cheti cha NABL
  • Wataalamu katika Nyanja za Transplants, Cardiac sciences (Cardiology & Cardio-thoracic Surgery), naNeurological sciences (Neurology &Neuro-surgery)
  • Maabara kubwa ya Sleep Lab katika bara la Asia
  • Moja kati ya Wodi kubwa ya Dialysis nchini India
  • Kituo cha Kansa cha Apollo kinafaa kamili kwa ajili ya Kushughulika ugonjwa wa Kansa. Kituo cha Radiation Oncology kinatoa huduma za NovalisTx, ClinaciX na HDR-Brachytherapy
  • Wodi ya Upandikizaji wa Uloto au Bone Marrow Transplant Unit ina viwango vya hali ya juu vinavyosaidia kuzuia maambuzi ya aina yoyote kushambulia
  • PET-MR, PET-CT, Da Vinci Robotic Surgery System, Brain Lab Navigation System, Portable CT Scanner, NovalisTx, Tilting MRI, Cobalt based HDR Brachytherapy, DSA Lab, Hyperbaric Chamber, Fibroscan, Endosonography, 3 Tesla MRI, 128 Slice CT scanner, mashine zote hizo hutumiwa kutoa huduma za kisasa za afya.

Katika Hospitali za Apollo tunaelewa kuwa kutafuta matibabu nje ya nchi yako ni jambo linaloweza kukuhangaisha sana na kukusumbua kimawazo lakini tutakusaidia kupunguza hali hiyo. Turuhusu tukusaidie kupanga pamoja nawe safari kwa kujaza fomu iliyo upande wa kulia ili Msaidizi wetu wa Kimataifa akusaidie.

Indraprastha Apollo Hospitals

Address: Sarita Vihar,
Delhi Mathura Road,
New Delhi - 110076 (INDIA)

Languages

Talk to Our International Representative form

logo
Patients Speak
Ms. Devanayagi, Chennai

Ms. Devanayagi came to Apollo Hospitals Chennai in 2014 for a complicated surgery; combined heart and double lung transplant.